Katika Petro wa Pili tunajifunza kwamba neema na amani zaweza kuzidishwa kwetu kwa kumjua Mungu na Yesu Kristo Bwana wetu. Tunaweza kuja katika mwelekeo wa mbinguni na katika ujuzi wa Mungu, na Yeye hutupa kila kitu tunachohitaji kwa maisha na utauwa. Petro anaeleza jinsi, tunapoifikia Nuru ya Neno, na kutumia Neno Lake maishani mwetu, Nyota ya Asubuhi inachomoza ndani ya mioyo yetu na Kristo anazaliwa ndani yetu.
Toa Jibu
Ni lazima uingie ndani kutuma maoni.