Waebrania – Ufunuo
Wakati mwingine huitwa “Kazi Bora ya Ajabu,” sehemu hii huanza na kitabu cha Waebrania, kitabu ambacho kinaunganisha Agano la Kale na Agano Jipya kuliko kitabu kingine chochote katika Biblia. Kitabu cha Waebrania kinamwonyesha Yesu Kristo kama Masihi ambaye alitabiriwa katika Agano la Kale, kama Bwana Ambaye alifunuliwa katika Agano Jipya na kama Mfalme wa wafalme ambaye atakuja tena. Sehemu hii pia ina kile kinachoitwa “nyaraka za jumla.” Zinaitwa “jumla” kwa sababu hazielekezwi kwa kanisa, jiji, au mtu mmoja hususa lakini zimeandikwa kwa kanisa kwa ujumla. Hizi pia kama barua za Paulo zina maagizo muhimu kwa afya ya kimungu ya kanisa. Mwishowe, sehemu hii inahitimishwa na kitabu cha Ufunuo. Sehemu kubwa ya kitabu hiki ina maono ambayo mtume Yohana alikuwa nayo wakati wa uhamisho huko Patmo. Mungu alimpa Yohana maono haya ya kile kitakachokuja mwisho wa vitu vyote. Ufunuo umejaa taswira na ufananisho na ni vigumu kuelewa; hata hivyo, ni kitabu muhimu na kinawahimiza waumini kujua kwamba mwishowe Mungu atashinda maadui Wake na watu wa Mungu wataishi milele pamoja Naye.
Comments are closed.